WATU 14 ambao ni ndugu wa familia moja waliokuwa wakielekea katika shughuli za mahafali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Msata kambi ya Kihangaiko leo, wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mchanga lenye namba za usajili T 439 DCC katika Kijiji cha Dundani wilayani Mkuranga.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, mkoani Pwani, Onesmo Lyanga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali ni dereva wa lori aliyekuwa amesinzia.
Taarifa zaidi tutawaletea baadaye, endelea kufuatilia mitandao yetu…..
CREDIT: ITV