Mapacha walioungana (Maria na Consolata) wamefariki dunia usiku huu wa Jumamosi Juni 2, 2018 katika hospitali ya Iringa walikokuwa wakitibiwa.
Mapacha Hawa walifanikiwa kuanza masomo yao ya juu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Ruco) cha mjini Iringa mwaka jana baada ya kufaulu vizuri masomo yao ya kidato cha sita.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Richard Kasesela amethibitisha kupkoea taarifa za msiba huo.
Tangu mwishoni mwa mwaka jana, mapacha hao walifanyiwa uchunguzi mara kadhaa baada ya kupata matatizo ya moyo.
Mapacha hao waliwahi kulazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu wakitolewa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.