Sasa kazi imeanza unaweza kusema , ikumbukwe kuwa ni siku kadhaa zimepita tangu mtandao huu (massheleblog) kupitia makala yake ya kilio cha haki kuchapisha kero hii
https://masshele.blogspot.com/2018/05/tcra-mitandao-ya-simu-jeshi-la-polisi.html?m=1Sasa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Barnabas Mwakalukwa, leo Juni 6, imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa kwani jumbe hizo zina lengo la kuwatapeli na kuwaibia fedha wananchi.
“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi... sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto.’