
Matukio ya ajali za barabarani nchini yameendelea kuteketeza maisha ya Watanzania, baada ya leo June 6, 2018 majira ya asubuhi, Watu 12 kufa papo hapo katika ajali iliyohusisha basi na treni ya Mizigo katika makutano ya reli eneo la Gungu, Manispaa ya Kigoma mkoani Kigoma.
Basi hilo la Princes Amida linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Tabora limegongana na Gari Moshi ( treni ) na kusababisha Majeruhi waliopo hospitali ya Maweni ni 28 na 4 wameripotiwa kuwa katika hali mbaya.
Katika ukurasa wake wa kijamii wa Facebook,Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe.Zitto Kabwe ameungana naWanakigoma kuwatakia majeruhi waliopo hospitalini Mola awape nafuu ya kupona haraka na kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu.
Taarifa Zaidi juu ya ajali hii endelea Kutembelea hapa. Masshele blog-Picha Na Adrian Eustus – Kigoma.
Hapa chini ni sehemu ya Picha za Ajali hiyo.










