Wednesday

MAKONDA AWAMWAGA SUMA JKT MTAANI, WATUPA UCHAFU KUSHUGHULIKIWA

0 comments


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, leo ametangaza kuanza kwa oparesheni kabambe ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira kuanzia Jula Mosi mwaka huu  kwa lengo la kuhakikisha jiji lake linakuwa kwenye hali ya usafi kama majiji mengine ulimwenguni.

Makonda amesema ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa (JKT) ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.

Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi ambapo  ameamua kuwachukuwa kwaajili ya kufanya kazi hiyo na kwenye kiasi cha faini watakazo watoza  wachafuzi wa mazingira 40% itaenda kwa vijana hao na 60% itaelekezwa serikalini.

Makonda amesema hawezi kukubali kuona jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.

Itakumbukwa hivi karibuni Rais Magufuli alifanya usafi kama sehemu ya kuhimiza usafi lakini bado watu wamekaidi, pia ulianzishwa utaratibu wa usafi kila jumamosi watu wasifungue maduka hadi wafanye usafi lakini bado pia wamekaidi jambo ambalo Makonda ameamua sasa kuja na mkakati wa kuwatumia vijana wa JKT  kufanya jukumu la kuwakamata wachafuzi wa mazingira.