Tuesday

AJALI YAUA WANAFUNZI, DEREVA, UDSM

0 comments

AJALI mbaya imetokea usiku huu wa Jumatatu, Juni 11, 2018 katika maeneo ya Ubungo Riverside jijini Dar es Salaam ambapo gari la wagonjwa (ambulance) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iliyokuwa ikipeleka mgonjwa katika hospital ya Kampasi ya Mlimani ikitokea Hosteli za Mabibo, inadaiwa kugongana na lori aina ya scania.
Katika tukio hilo, inadaiwa watu watatu wamepoteza maisha papo hapo, hata hivyo    majina  ya walio 
Fariki hayakufahamika mara moja. Lakini baadaye tuliweza kupokea taarifa ifuatayo kutoka katika mamlaka husika 


TAARIFA KWA UMMA

Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kupitia Wizara ya Afya na Kafteria imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya ajali mbaya iliyotokea siku ya *_11 June, 2018 majira ya saa tatu usiku maeneo ya Riverside_*

Ajali hiyo imehusisha Ambulance ya Chuo iliyokuwa na watu wafuatao 
*1.Soko, Maria Godian(student)*
*2. Steven E Sango (student)*
*3. Abishai Nkiko (student)*
*4.James (driver)*

Hadi sasa wanafunzi wawili ambao ni *_Soko, Maria Godian (first year Coss) na Steven E Sango  (CPE CoET second year) pamoja na James (dereva)_* wamefariki dunia 

*_Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe._*

MUNGU azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amina.

Mwanafunzi mwingine *_Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering third year CoET)_* hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tuendelee kumuombea apate kupona haraka.

*_Imetolewa na Wizara ya Afya na Kafteria_*

*Kodi, John H.*- Kaimu Waziri 0755659514

*Enock, Charles*- Naibu waziri 0768872704

*_UNITED WE STAND DIVIDED WE FALL_*

  *_12 June, 2018_*

  *_@DARUSO 2017/2018_*