Na VICTORY M.
Huu ni wakati wakuchagua viongozi mbalimbali katika chuo kikuu cha Dar es salaam na ndaki mbalimbali Mambo yamepamba moto huku kila mgombea aki omba kura kwa udi na uvumba pamoja na kuahidi mambo mbalimbali
Katika ndaki ya IKS Mambo ni moto asikwambie mtu
Katika online exclusive interview, iliyo fanyika kwa vipindi tofauti baadhi ya Wagombea walileta sera na ahadi zao
Na hapa nimekuwekea kila kitu
Mgombea namba moja alikuwa ni
RAMADHANI MZAVA, MGOMBEA UKATIBU IKS
Mgombea huyu vipengengele vyake alivyo vipa kipaumbele
1 . Suala la taaluma hasa changamoto za matokeo na changamoto ya mpangilio mbovu wa ratiba
2 . Amezungumzia suala la umoja na mshikamano
3. Kwa mgombea huyu michezo haijaachwa nyuma pia kaipa kipaumbele.
OJWANG HAPPINES
Mgombea viti maalum Iks
Mgombea huyu Vipaumbele vyake ni
1. Uwakilishi mzuri na imara katika nafasi aliyo omba
2 Uhamasishaji hasa maswala yaykimichezo na nk
4. Utatuzi wa matatizo ya kijinsia
5. Ushirikiano wa kutosha
HASHIM JUMA,
mgombea nafasi ya mwenyekiti IKS
mgombea nafasi ya mwenyekiti IKS
Mgombea huyu Vipaumbele vyake ni
1.Kutatua changamoto za ucheleweshwaji wa matokeo
2. Kuhakikisha wanafunzi wa IKS wanapata vifaa vya kusomea, videsa, notes nk.
3. Ushirikiano katika maswala ya kijamii na ufwatiliaji
4. Umoja
Pia nilifanikiwa kumuuliza swali mgombea huyu.
"Swali
huenda mimi au mwingine anapenda kujua umejipanga vipi kikabiliana na cha
Ngamoto mbalimbali ambazo zipo au zitakuwepo katika uongozi wako
Jibu
OK poa so changamoto kubwa kwtu kitaaluma ni kucheleweshwa kwa matokeo hivyo utatuzi ni kwamba kushirikiana kwa karibu na ARIS UNIT pamoja na EXAMINATION OFFICER WA TATAKI ili yatoke kwa muda muafaka.
GABRIEL MWABUPINA
Mgombea nafasi Mwenyekiti IKS alikuwa na Vipaumbele vifuatavyo
1. Suala la taaluma kwa kushirikiana na viongozi wa madarasa
2. Uwajibikaji wa kutosha na utekelezaji wa majukumu ipasavyo.
3. Michezo na sanaa kwake hatoona shida kuiendeleza na kuhamasisha
Pia mgombea huyu ameapa kutokuwa mungu mtu kwa wale atakao waongoza.
JOSEPH THEOGENENS
Mgombea huyu Vipaumbele vyake ni
1. Suala la taarifa mbalimbali yani kuwaweka watu update na kila kinacho endelea
2. Taaluma /elimu hapa ametilia mkazo swala la ucheleweshwaji wa matokeo, Pia kuhusu muainisho mzuri wa kozi
3. Ufuatliliaji hasa fedha zinazodaiwa kuwa ni za utafiti, Na maswala ya mikopo, pia ufuatiliaji wa maswala ya field
5. Michezo na umoja
mgombea huyu haamini katika maneno tu pasi na utendaji
Utendaji kwake Ndio kipaumbele
"Nimeamua kuwania nafasi ya kuwa mwenyekiti kwa sababu naamin uongozi ni wito na wito huu unajidhihirisha pale unapojitolea katika mambo mbalimbali
Nyote ni watu waelewa hivyo nawaomba mfanye maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi wanaofaa kuiongoza taasisi yetu.
naamini kiongozi anatakiwa kuwasaidia watu anao waongoza kwa hali na mali. Hivyo naamin bila umoja na ushirikiano hakuna kitu chochote kinacho weza kufanyia.
Sifikirii kuwadanganya kwa ahadi za kufikilika kwa sababu Naamini nyie ni watu waelewa na mnajua nani anafaa kuwa mwenyekiti.
Siamini katika neno nitafanya, nitawapa, nitatekeleza, kwangu hayo ni maneno ya ushawishi tu kwa sababu ukiwa kama mwenyekiti bado unakuwa chini ya uongozi wa Tataki hivyo kuwaaminisha kuwa nitatekeleza vitu kadha wa kadha sio kweli.
Siamini katika utengano kama unawiwa na kumchagua Juma kama kiongozi fanya hivyo, mwabupina pia, fanya hivyo kwa sababu wote ni ndugu na tuna lengo moja.
2. Pia mgombea huyu ameahidi mshahara mnono kwa kila mwakilishi wa darasa
Mwenyekiti nae katoa neno
Aidha aliyekuwa mwenyekiti wa zamani Youze Hoza amewataka wapigakura kuhakikisha wanajitokeza na kupiga kura siku ya uchaguzi.
Muhimu
hao ni baadhi ya Wagombea nilio fanikiwa kuzungumza nao mawili matatu ambao hujawaona kutokana na majukumu imeahindikana lakini tukijaaliwa utakuwa nao insh allah
Tahadhari
Sera zilizo andikwa hapa ni baadhi tu hivyo jukumu lako nikuwasikiliza Wagombea na kufanya maamuzi sahihi