Dodoma. Mhadhiri wa Chuo cha Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mdenye ameuawa kwa madai ya kuchomwa kisu na mumewe usiku wa kuamkia leo Mei 26.
Akizungumza na MCL leo asubuhi, Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Beatriece Mtenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Mtenga amesema msiba upo Kisasa Sheli.
Credit mwananchi