Media za kujifunzia na kufundishia hutegemeana na stadi ambayo mjifunzaji anataka kuifahamu, au mfundishaji anayohitaji kufundisha mfano + Kusikiliza +Kuzungumza +kusoma +kuandika nk
kwamfano ikiwa utahitaji kufundisha stadi ya kusoma unaweza kutumia tovuti, kusikiliza, unaweza kutumia 📺 TV. Radio YouTube, (audio)
2.1 Vielezo na teknolojia kwa kufundishia na kujifunzia
2.2 Upatikanaji wa vielelezo na teknolojia
2.3 Faida na hasara za matumizi ya media za kisasa katika kufundishia
2.3 Faida na hasara za matumizi ya media za kisasa katika kufundishia
DHANA NA MAANA YA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Ni jumla ya zana au vifaa ikiwa ni asilia au vya kisasa vinavyoweza kutumiwa na mwalimu katika ufundishaji na kumsaidia kufundisha mada husika kwa ufanisi zaidi na mwanafunzi kuelewa mada hiyo kwa urahisi.
Mfano tufe,matunda,komputa,redio,projecta,vifani mbalimbali nk.
SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
i. Viwe sahihi katika muundo wake na kwa matumizi. Hii ina maana iwe na mjengo uliorahisi kuonekana, kupangwa na kupanguliwa
ii. Viwe na ukubwa unaofaa. Hii ina maana zana iwe na ukubwa wa kati, kama ni chombo cha sauti, pia kiwe na sauti ya kati
iii. Viwe na mvuto,ili kuvuta usikivu kwa walengwa.
iv. Vishabihiane na ujumbe uliokusudiwa
v. Vizingatie umri na uelewa wa walengwa
vi. Viwe imara na vya kudumu
vii. Visiwe na uwezo wa kupotosha dhana iliyokusudiwa
viii. Viendane na mazingira halisi ya watoto
ix. Vihamishike/viwe rahisi kubebeka.
NJIA ZA UPATIKANAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Vielelezo vya kufundishia na kujifunzia vinaweza kupatikana katika njia kuu zifuatazo:
i. Kununuliwa.Mfano: Komputa,magazeti,redio,tepurekoda,projekta nk
ii. Kuazima.Mfano:-Kompyuta,projekta nk.
iii. Kuchukua/kutayarishwa kutoka mahali vilipohifadhiwa
iv. Kutengenezwa/kufaraguliwa,kama vile:-vifani vya viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama vile mche duara,mche mstatili,tufe nk.
Hasara za baadhi ya vielelezo ni gharama kuvinunua, nivigumu kutumiwa , nivigumu kuendeshea, rahisi kuharibika kama havitohifadhiwa vizuri
Faida
Huhifadhi kwa mudamrefu, huvutia, humpunguzia mzigo mwalimu, huweza kufundishia hata walioko mbali, hukuza technolojia nk
Asante kwa kusomea masshele blog