MICHUANO ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Juni 3 jijini Nairobi na mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wanatarajiwa kuondoka saa 12 asubuhi ya leo Alhamisi na kikosi kamili kwenda kusaka tiketi ya kucheza na Everton nchini Uingereza
Ukimuondoa Haruna Niyonzima, Simba itawakosa nyota wake wengine wote wa kigeni pamoja na nahodha John Bocco huku akijumuishwa mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea, Marcel Kaheza. Taarifa zinadai Adam Salamba anatarajiwa kuungana na wenzake Jumamosi hii.