Saturday

OMARY NONDO ATWAA TUZO MUHIMU YA MTETEZI KIJANA CHIPUKIZI WA HAKI ZA WANADAMU

0 comments


Omary Nondo ambaye ni mwanafunzi wa UDSM na mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi tanzania TSNP, ame twaa tuzo muhimu ya
mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu. Ikumbukwe kuwa Nondo alikuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanafunzi hasa kudai walio husika na kifo cha Mwanafunzi Akwilina kuwajibishwa

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii NONDO ameandika yafutwayo
Kwanza namshukuru Mwenyezimungu kwa kunipa Afya njema, pia wazazi wangu na viongozi wenzangu wa TSNP na watanzania wote kwa ujumla kwa faraja zao na matumaini yao kwangu.

Napenda kutoa shukrani zangu za Dhati kwa Mtandao wa watetezi wa haki Za Binadamu Tanzania. (THRDC) kwa kutambua mchango wetu TSNP kwa kunizawadia Tuzo kama  mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu (wanafunzi) Tanzania Nimefarijika saana.

TSNP pia tumekuwa tukitetea haki za wanafunzi kwa kushirikiana pia na baadhi ya taasisi za kiserikali, wizara ya elimu,wizara ya Tamisemi ,bodi ya mikopo na Tume ya vyuo vikuu zimekuwa zikisikia na kutatua shida za wanafunzi ambazo tumekuwa tukizisemea.

Tuzo hii ina maana kubwa kwangu na viongozi wa TSNP.

Ina maana kubwa ya kuinua hari mpya ya kusemea na kutetea haki za wanafunzi Tanzania katika maswala mbalimbali.

Tuzo hii ina maana kuwa changamoto zipo katika sekta yeyote, ila jambo kubwa ni kuwa mvumilivu, mstahimilivu na kutambua kuwa changamoto haziepukiki katika majukumu haya,na kutokubali changamoto hizi kudhoofisha utetezi wa wanafunzi na kurudi nyuma.

TSNP tutaendelea kushirikiana na taasisi zote za kiserikali na Taasisi zote zisizo za kiserikali katika kutetea na kusemea shida na haki za wanafunzi Tanzania ili wapate haki zao zitakazowezesha Taifa letu kuwa na viongozi na wataalamu kwa maendeleo ya taifa letu.

Shukrani THRDC, Shukrani LHRC, Shukrani TSNP, Shukrani Watanzania wote.

Abdul Omar Nondo.

Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP).