Lugha ya Kiswahili inaonekana kuzidi kukuwa na kuwavutia watu mbalimbali dunia kuitumia, leo April 1 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo Georgina Rodríguezambaye ni mpenzi wa staa wa soka waReal Madrid Cristiano Ronaldo.
Georgina Rodríguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina, hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika‘Hakuna Matata’
Msemo wa hakuna matata ni msemo waKiswahili ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado Georgina Rodríguez ameujulia wapi msemo huo.