Tohara (kutoka Kiarabu: طهارة tahara - safi, tahiri) ni upasuaji mdogo wa kukata na kuondoa govi, yaani ngozi inayofunika ncha ya uume.
Wakati mwingine ukeketaji huitwa "tohara ya mwanamke", lakini matumizi hayo si sahihi, kwa sababu ni aina tofauti za upasuaji, ingawa zote mbili zinahusu viungo vya uzazi.
Tohara inaweza kufanyika katika umri wowote na kwa sababu za kiutamaduni, za kidini au za kiganga. Mara nyingi desturi za kutahiri zinachanganya sababu za kidini na za kiutamaduni. Kwa mfano, Waislamu wa Misri huamini ya kwamba wanatahiri watoto wao kama amri ya kidini lakini Wakristo Wakopti wa nchi hiyo hutahiri watoto vilevile. Ukweli ni kwamba tohara ilikuwa desturi ya Wamisri tangu kale.
Tohara inafanyika hasa mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto au wakati wa kubalehe.
Kufuatana na Shirika la Afya Duniani takriban 30% za wanaume wote duniani wametahiriwa,
Tohara na dini
Uyahudi
Kwa Wayahudi tohara ni ishara ya agano lao na Mungu na inapaswa kufanyika siku ya nane baada ya mtoto wa kiume kuzaliwa ili kumwingiza mapema katika taifa la Mungu.
Kufuatana na habari za Biblia (Mwanzo 17), Ibrahimu alikuwa mtu wa kwanza kupokea amri ya kutahiriwa kama alama ya agano.
Ukristo
Yesu mwenyewe alitahiriwa siku ya nane kama Wayahudi wote wa kiume. Tohara ya Yesu inakumbukwa kwa sikukuu maalumu katika makanisa mengi duniani hasa Waorthodoksi, pia kwa sababu ilikuwa ndiyo siku ya kupewa rasmi jina lake hilo.
Agano Jipya linaonyesha jinsi gani suala la tohara lilikuwa motomoto mwanzoni mwa Kanisa, wakati Wakristo wengi walitoka katika Uyahudi.
Kufuatana na kitabu cha Matendo ya Mitume (15:23-29) Mtaguso wa Mitume uliofanyika Yerusalemu uliamua Wakristo kutoka mataifa wasilazimishwe kutahiriwa.
Hasa Mtume Paulo alisisitiza kwamba jambo hilo si muhimu tena, cha maana ni kuwa watu wapya kwa imani.
"Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya" (Waraka kwa Wagalatia 6:15).
"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili" (Waraka kwa Wafilipi 3:3).
Hata hivyo Wakopti wa Misri na Ethiopia wameendelea kutahiri watoto wao.
Uislamu
Katika Uislamu tohara hufundishwa kama wajibu wa kidini kwa kila mwanamume.
Hakuna amri katika Kurani kuhusu tohara lakini inatazamwa kama sunna ya mtume Muhamad. Kwa imani hiyo ni ishara ya mitume ya kwamba walizaliwa bila govi katika hali ya kutahiriwa tayari.
Utekelezaji wa tohara huwa tofauti kati ya nchi na nchi; mara nyingi mtoto hutahiriwa akiwa na umri wa miaka 5 hadi 10. Katika mazingira ya mjini wazazi wanawahi kumtahiri mapema.
FAIDA TOHARA KIAFYA
1. USAFI, Kikawaida Ngozi ya uume( govi) huficha uchafu na pia kuzalisha mafuta meupe meupe yanayojulikana kitaalamu kama smegma ambayo huweka mazingira ya wadudud (bacteria kuzaliana) hivyo kusababisha maginjwa
2.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Mtu anapotahili ngozi ya kichwa cha uume huwa ngumu na kuzuia kupata michubuko kiurahisi tofauti na ya mtu ambaye hajatahili hivyo kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kiasi fulani.
3.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAGONJWA ZA ZINAA NA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO
4.KINGA DHIDI YA SARATANI YA UUME(PENIS CANCER)
utafitiu unaonesha kua saratani ya uume inawapata sana watu ambao hawajatahili
5.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE
Utafiti pia unaonesha kua mwanamke kujamiiana na mtu ambaye hajatahili inamweka kwenye hatari( Risk )ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kutokana na uchafu unaotunzwa kwenye govi kuweza kua na Virusi aina ya Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo husababisha saratani ya shingo ya kizazi.