Video vixen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde katika Hospitali ya Mama Ngoma ya jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.
Dkt. Kihama Ngoma ameithibitishia Masshele blog .
Taarifa zaidi
Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.
Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.
Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017.