Wednesday

OMARY NONDO MWENYEKITI TSPN NA MWANAFUZI UDSM KATEKWA?

0 comments

Taarifa nilizozipata zinaeleza kuwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha DSM Na mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi TSNP #ABDUL_NONDO  hajulikani alipo na huenda akawa ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa jana.


Abdul Nondo ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania hajulikani alipo na simu yake ya mkono haipatikani mpaka muda huu....

Inaelezwa kuwa kabla ya kupotea kwa kiongozi huyu mkubwa wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania alimtumia meseji yenye utata rafiki yake iliyokuwa ikionyesha yupo kwenye hatari,... Nanukuu  "At at risk".

 Inaelezwa kuwa baada  kumtumia rafiki yake meseji hiyo alipotafutwa na  kumtafuta kwa njia ya simu yake ya kiganjani simu yake iliita bila kupokelewa na baadaye kuzimwa.

Nimewasiliana na baadhi ya viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi wamenieleza kuwa wanaendelea kufuatilia ni wapi alipo kiongozi huyu na wamenieleza kuwa wapo njiani kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.

Je Kiongozi huyu atakuwa wapi???.... Je atakuwa ametekwa??

Tutaendelea kuwajuza.