YANGA SC watateremka dimbani Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Februari 25, mwaka huu kumenyana na Maji Maji ya Songea katika mchezo wa hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba mechi za hatua ya 16 Bora ya ASFC zitafanyika kati ya Februari 21 na 26, mwaka huu.
Tayari timu hizo zimekwishakutana mara mbili msimu huu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 16, mwaka jana zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na jana Yanga ikishinda 4-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TFF imesema imekwishafanya ukaguzi wa Viwanja vitakavyotumika kwenye raundi hiyo ya nne ya michuano hiyo, ambayo bingwa wake mtetezi, Simba SC alikwisahtolewa hatua ya 62, sawa na Raundi ya Pili kwa kufungwa penalti na Green Warriors ya Daraja la Pili, baada ya sare ya 1-1. Green Warriors nayo ilitolewa na Singida United hatua iliyopita, ya timu 32.
TFF imesema baada ya ukaguzi huo sasa JKT Tanzania watatumia Uwanja wa Azam Complex kwa mchezo wake dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara wakati Kiluvya United watatumia Uwanja wa Mabatini Mlandizi kwa mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons.
Michezo hiyo imehamishwa kwasababu ya viwanja hivyo kutokidhi viwango vya kikanuni baada ya wataalamu kutoka idara ya Ufundi TFF kufanya ukaguzi.
“Ifahamike kuwa kanuni ya 7(7) ya ASFC inatamka kuwa TFF ina mamlaka ya mwisho kuhamisha mchezo husika katika Uwanja mwingine au kubadilisha kituo cha mchezo kwasababu inazoona zinafaa kwa mchezo na wakati husika,”imesema taarifa ya TFF.
Kwa mujibu wa Ratiba, Februari 21 kutakuwa na mchezo utakaowakutanisha Njombe Mji vs Mbao FC utakaochezwa Uwanja wa Sabasaba Njombe,Februari 24 Singida United watakuwa Uwanja wa Namfua Singida kucheza dhidi ya Polisi Tanzania saa 10 jioni wakati KMC watacheza dhidi ya Azam FC saa 1 usiku Azam Complex,Chamazi.
Mechi nyingine zitachezwa Februari 25 wakati Buseresere watakapowakaribisha Mtibwa Sugar saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Nyamgana nao Majimaji FC ya Songea watakuwa Uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Yanga SC Saa 10 jioni na saa 1 usiku Azam Complex JKT Tanzania watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara.
Februari 26 Kiluvya United watawakaribisha Tanzania Prisons kutoka Mbeya uwanja wa Mabatini saa 8 mchana na Kambarage pale Shinyanga Stand United watacheza na Dodoma FC saa 10 jioni

Tangazo.