Saturday

PICHA ZILIZO ITIKIZA DUNIA

0 comments
Kazi ya uandishi wa habari ni moja ya kazi yenye changamoto sana. Waandishi wengi wamekuwa wakilaumiwa kwa kazi zao na kuonekana kama watu wasio na utu, kwa kuweka kazi zao mbele kuliko ubinadamu.
Picha hii ilipigwa mwaka 1992 nchini Somalia, ikimuonesha mama akiwa amebeba maiti ya mtoto wake aliyekufa kwa njaa.
Hapa nakuletea baadhi ya picha zilizopigwa na waandishi tofauti tofauti duniani kwenye majanga mbali mbali na kufanya dunia nzima ielekeze macho yake kwenye suala hilo, na baadhi zikiweza kuwapa tuzo waandishi waliopiga picha hizo.
Picha hii ilipigwa na mpiga picha Kevin Carter nchini Sudan wakati wa janga la njaa mwaka 1993. Ilipokuwa published dunia nzima ilishtushwa nayo na Umoja wa Mataifa kuzidi kutia nguvu kwenye janga hilo. Picha inamuonyesha ndege akiwa anamsubiria mtoto aliyekuwa na njaa afe ili aweze kumla. Picha hii ilimpa Tuzo ya Pulitzer Kevin na kuzidi kumpa umaarufu duniani, lakini ikawa ni moja ya tukio ambalo lilipelekea mwandishi huyo kujiua.

Picha hii ilipigwa mwaka 1984 na Pablo Bartholomew baada ya mlipuko wa bomba la gesi nchini India lilisababisha kuua watu elfu 15 na kuathiri wengine zaidi ya laki 5. Mpiga picha alimnasa baba akimzika mtoto wake aliyekufa baada ya kuvuta gesi hiyo.
Mwaka 1985 volcano ililipuka huko Columbia na kuteketeza kijiji cha Armero. Miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ni binti Omayra Sanchez aliyekuwa na miaka 13. Mpiga picha Frank Fournier alimpiga picha hii akiwa amekwama kwenye matope, majivu na maji. Waokoaji walijaribu kumtoa lakini waligundua kuwa miguu yake imekwama kwenye paa la nyumba yao iliyokuwa imebomolewa na volcano, na chini yake kulikuwa na maiti ya shangazi yake ambaye alifariki. hivyo kumtoa bila kujeruhi isingewezekana, Walimuwekea mpira ili asizame huku wakendelea kutafuta njia mbadala ya kumtoa, walikuwa wakihofia iwapo watamtoa lazima watamvunja miguu na huduma za afya hazikuwa zenye ubora. Aliwaambia waokoaji wamuache wapumzike na kumuomba mpiga picha ampe chakula kitamu na soda. Omayra alifariki baada ya kukaa kwa siku tatu kwenye tope hilo.
Picha hii ilipigwa na Mike Wells katika eneo la Karamoja nchini Uganda mwaka 1980, ikimuosha mmishenary akiw ameshika mkono wa mtoto aliyekonda kutokana na njaa ambayo ilikuwa inaikumba Uganda kwa kipindi hiko. Picha ilitumwa kwa ajili ya kuwa published lakini haikuwekwa kwenye habari, na badala yake iliingizwa kwenye shindano la picha na kumpa tuzo ya picha bora ya mwaka ya habari.
Picha hii ambayo ilizunguka kwenye mitandao na kila chombo cha habari na kushtua dunia nzima mnamo mwaka 2015, ilipigwa na Nilufer Demir ikimuonyesha mtoto mwenye asili ya Syria akiwa amekufa maji, baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kuzama katika pwani ya Syria, wakielekea Ulaya. Maelfu ya watu hupoteza maisha yao baharini kutokana na kujaribu kuvuka kwa boti kwenda Ulaya kama wahamiaji haramu.
Picha hii ilipigwa mwaka 2006 na mpiga picha Oded Balilty na kuchukua tuzo ya Pulitzer, ikimuonesha mwanamke wa kiyahudi akipambana na askari wa Israel katika mji wa Ramallah uliopo Mashariki mwa Palestina.