Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi yenye madarasa ya awali na kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano na cha sita.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jana Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.