Wednesday

Wanafunzi Zaidi 1500 Wa Tanzania Wapata Nafasi Kusoma China

0 comments
Kampuni  ya Elimu solution imeungana na ubalozi wa china uliopo Tanzania kupinga na kukemea makampuni yanayotoa nafasi za masomo ya nje kwa wanafunzi wa Tanzania kufanya kazi katika mfumo usiokuwa na utaratibu ambao hauzingatii vigezo na masharti.

Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa Elimu solution Neithan H. Swedy amesema na kusisitiza kuwa kuna uwepo mkubwa wa makampuni ambayo hayafanyi kazi kwa usahihi na kuwataka waweke wazi utaratibu mzima wa utendaji kazi wao.

“Elimu Solution tunasisitiza kuwa kuna uwepo mkubwa wa kampuni ambazo zinafanya kazi kwa kupindapinda na  hata kuchukua ada kwa baadhi ya wanafunzi” amesema Swedy.

Aidha pia Swedy amesema kuwa Elimu solution imezindua rasmi udahili wa wanafunzi wa Elimu ya nje kwa mwaka 2018 na kufafanua kuwa udahili huo utakuwa katika awamu tatu ambazo ni Machi, julai na disemba.

Akifafanua namna ya kufanya udahili kupitia elimu solution, Swedy amesema kuwa zipo njia mbili ambazo watazitumia ambapo ni online pamoja na Physical na kuongeza kuwa wanafunzi watakaotumia njia ya online watatumia website ya www.elimu solution.com.tz. ambapo itakuwa inajieleza kila kitu na mtu anaweza akauliza chochote na kujibiwa papo kwa hapo.

Pia amesema kuwa kutokana na maombi ya wanafunzi mbalimbali kuomba kuongezewa nchi nyingine ambapo awali Elimu solution walikuwa wakifanya kazi na China tu, Sasa wamefanikiwa kuongeza nchi nyingine mbili ambazo ni Japan na south Korea.

Pia Swedy amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa sekta ya elimu nchini kwani takribani wanafunzi 1500 wana uwezekano wa kupata udhamini wa kusoma nje ya nchi na kuongeza kuwa mpaka Sasa Wapo wanafunzi 132 nje ya nchi.

Pia amesema kuwa zipo ofa mbalimbali ambazo zitatolewa na vyuo lakini ni kwa wanafunzi wanaosoma Masters na Phd ambapo ofa hizo ni malazi, ada pamoja na mshahara usiopungua shilingi 300, 000 na kuendelea.

Lakini pia Swedy amewatoa wasiwasi wanafunzi wasiokuwa na uwezo na kusema kuwa kwa Sasa  baadhi ya vyuo vya nje vinadai ada Sawa na vyuo vikuu vingine vya Tanzania na kusisitiza kuwa hata hiyo ni katika vyuo washirika wa taassisi ya Elimu Solutions hiyo ni moja ya ofa ambayo inatolewa na vyuo hivyo.

Bw. Swedy amesema  taasisi ya Solutions (T) Limited ni mawakala rafiki wa kisheria wa vyuo zaidi 300 kutoka nchi za china, Japan na Korea Kusuni na kutokana na  mahusiano mazuri taasisi hiyo imeweza ,  kuhakikishiwa kupata nafasi zaidi ya 1500 za masomo(Scholarships) kwa kila muhula mpya wa masomo  kila ngazi za masomo  kwenye vyuo  washirika wetu.

Ameongeza pia  kwamba dhamira kuu  ni kuutaarifu umma kuhusu ufunguzi wa muhula mpya wa masomo kwa mfumo wa udhamini (Scholarship) kwa ngazi Astashahada(Mastares and Phd) Uzinduzi wa tovuti (Website) ya kisasa na Programu( Mobile Application pamoja na taratibu na mifumo bora ya utendaji wa kazi ndani na nje ya nchi na Ufunguzi wa mafunzo ya lugha kwa wanafunzi watakao pata nafasi za masomo katika vyuo hivyo.