Saturday

VITU VINAVOPELEKEA MTOTO KUPATA VIDONDA SEHEMU ZA SIRI KUTOKANA NA DIAPERS(DIAPER RASH)

0 comments


Diaper rash inaweza kusababishwa na chakula chochote kipya na mkojo wa mtoto mwenyewe. Hivi ni vitu ambavo ni adui wakubwa:

1. Unyevu unyevu.
Hata ikawa diaper zinanyonya kwa kiwango kikubwa kiasi gani hua zinaacha umaji maji katika ngozi ya mtoto wako. Na endapo mkojo wa mtoto wako ukichanganyika na bacteria kutoka katika kinyesi chake, bacteria hao hutengeneza ammonia,ambayo inaweza kua ni kali sana na kuunguza ngozi ya mtoto. Na ndio maana kwa watoto ambae hupata choo mara kwa mara ama kuharisha ni rahisi kwake kupata diaper rash..

Mtoto mwenye kuachwa na diaper chafu kwa mda mrefu ni rahisi kupata diaper rash, na mwenye ngozi nyeti(sensitive) anaweza kupata diaper rash hata kama mzazi atakua anafanya bidii kumbadilisha badilisha.

2. Mzio/chemical sensitivity.
Yawezekana mtoto wako akapata diaper rash kutokana na msuguano wa ngozi yake na diaper diaper aliovalishwa hasa kwa wale watoto wenye ngozi nyeti(Ngozi isiyokubaliana na baadhi ya vitu),chemical,manukato yaliyo katika diaper au sabuni inayotumika kuoshea nepi zake,pia diaper rash yaweza kusababishwa na lotion, powder unayompaka wakati unapomvalisha diaper yaweza isiendane na ngozi yake.

3. VYAKULA vipya
Ni kawaid kwa mtoto wakati wanapoanza kula vyakula vigumu(solid),chakula chochote kipya nacho hubadili asili ya kinyesi, acid ailiomo katika chakula hicho kama vile strawberries na juice nk yaweza kua ni tatizo kwa baadhi ya watoto. Chakula kipya chaweza kuongeza mtoto kupata choo mara kwa mara. Na kama unanyonyesha pia ngozi ya mtoto yaweza kuathirika na vitu unavokula.

4. MAAMBUKIZI
Diaper hupata joto na umajiumaji kama ambavyo bacteria na yeast wanavopenda kuishi sehemu kama hizo. Kwa hiyo ni rahisi kwa bacteria au yeast kuishi mahala hapo na kusababisha rash na zaidi katika sehemu zenye mikunjo kunjo ya ngozi . Baadhi ya watoto hupata tatizo la yeast infection.

5. MADAWA/Antibiotics. 
Mtoto na dawa za antibiotics, (au mtoto anayenyonya kwa mama alietumia antibiotic) wakati mwengine wanapata tatizo la yeast infection kwa sababu dawa hizo hupunguza nguvu za bacteria wa afya kushindwa kupigana na yeast na bacteria wabaya. Antibiotics pia zaweza kusababisha kuharisha kwa mtoto ambapo pia huchangia diaper rash.