Sunday

KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU WAKATI WA UJAUZITO (VARICOSE VEINS)

0 comments


Kuvimba kwa mishipa ya damu(Varicose veins) hasa miguuni ni kitu kinachowatokea mama wajawazito walio wengi.Tatizo hili mara nyingi hutokea wakati mimba imekua kubwa kuanzia miezi 8 hadi 9 japo kwa baadhi ya watu hali hii huweza kutokea katika umri mdogo.

Mishipa hii huvimba na inaweza kuonekana kwenye ngozi kama Mistari iliyovimba kwenye ngozi isiyoinyooka yenye rangi inaelekea kuwa kama blue.
Watu wanopata ujauzito katika umri mkubwa ndio wanakua kwenye hatari kubwa ya kutokewa na hali hii,pia watu wenye uzito kupita kiasi (wanene sana) wanakua kwenye hatari ya kukumbwa na hali hiii.

Hizi varicose veins zinatokea sana miguuni,ila zinaweza kutokea maeneo mengine kama kwenye uke na shingo ya kizazi,zinapotokea maeneo haya mama hutokwa na majimaji ukeni yaliyochanganyikana na damu. Varicose veins zinapotokea sehemu ya haja kubwa ndio tunaiita Bawasiri (Haemorrhoids)
Image result for varicose veins in pregnancy
DALILI ZA TATIZO HILI

Mistari myembamba yenye rangi ya blue inayoonekana kwenye ngozi
Uvimbe kwenye ngozi ambao si mgumu,ukiubonyeza unabonyea bila maumivu.
Unapo minya na kidole uvimbe unapotea ila unapotoa kidole unarudi
Muwasho kwenye sehemu zilizovimba

Zikitokea kwenye uke na shingo ya kizazi basi mtu hupata majimaji yaliyochanganyikana na damu,au kutokwa damu ukeni.

zikitokea sehemu ya haja kubwa mtu hupata maumivu wakati wa kujisaidia na kupata choo kilichochanganyikana na damu.

VISABABISHI VYA TATIZO HILI

1. Kutanuka kwa mji wa mimba.
Kadri mtoto anavokua tumboni,mji wa mimba (uterus) nao hutanuka hali inayopelekea kuibana mishipa ya damu inayotoa damu sehemu za miguuni kurudisha kwenye moyo na kusababisha damu kutoka kwenye miguu  kutotembea vizuri hivyo kupelekea mishipa (veins) kuvimba

2.Kuongezeka kwa kiwango cha hormone zinazosaidia kuimarisha mji wa mimba mfano hormone ya ESTROGEN na PROGESTERONE husababisha kuta za mishipa ya damu kuwa laini hivyo kuwa rahisi kuvimba.

3.Uzito mkubwa, Mtu anapokua na uzito mkubwa kupita kiasi inapelekea kuongeza shinikizo (pressure) kwenye miguu hivyo kupelekea mishipa ya miguuni kuvimba

4.Kutofanya mazoezi.

5.Kurithi, kuna baadhi ya watu wanarithi vinasaba vinavyowaweka kwenye hatari ya kupata tatizo hili la kuvimba kwa mishipa ya damu.

6.Kuzaa mara nyingi, wanawake waliozaa mara nyingi kuta za mishipa ya damu inakua iko dhaifu hivyo ni rahisi kuvimba.

7.Matatizo ya Vali (valves),Vali zinaluwa kwenye mishipa ya damu ikisaidia kufanya damu inapotembea isirudi nyuma,matatizo katika vali yanapelekea vali kushindwa kufanya kazi vzuri na kuruhusu damu kurudi chini na kupelekea mishipa ya damu kuvimba.


JINSI YA KUKABILIANA NA HALI HII

1.Unapolala weka mto miguuni ili kuinua kidogo juu miguu,hii husaidia kupunguza shinikizo(pressure) miguuni na kuzuia miguu kuvimba

2.Fanya mazoezi, mazaoezi husaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu.

3.Pata muda wa kupumzika.

4.Epuka nguo zinazobana hasa maeneo ya kiunoni na mapaja
5.Punguza uzito

FIKA HOSPITALI ILI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA MATATIZO MENGINE YANAYOPELEKEA HALI HII