Thursday

JESHI LA POLISI LAKANUSHA KUWAKAMATA WANAOVAA NGUO FUPI

0 comments
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa, hakuna agizo lolote lilitolewa na Polisi kuwakamata waliovaa nguo fupi amesema hayo baada ya habari iliyoandikwa katika gazeti la Nipashe la Januari 17, 2018 ‘Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku.
Mambosasa amesema hakuna sheria yoyote inayowazuia watu kuvaa nguo fupi na kwamba alichokisema Rais Magufuli ni kwamba anachukizwa na wasanii wanaovaa nusu uchi na kuoneshwa katika vituo vya Runinga,kitu ambacho ni kinyume na maadili yetu.
Kwa kuwa jambo hilo  ni machukizo na halivunji sheria za nchi ni Vigumu  kwa Polisi kuanzisha msako, labda watu hao tuwakute wakifanya biashara ya ukahaba.