Mtazamo wa sarufi miundo virai wa sasa kwa mujibu wa Chomsky
Mtazamo wa sasa wa sarufi miundo virai unazingatia dhanna ya umiliki na usabiki (utangulia), dhanna ambazo zinatawala mahusiano ya vipashio vya sentensi.
(a) Dhanna ya umiliki na usabiki:
Dhanna hizi zinajaribu kujibu maswali matatu ambayo ni maana,muundo na uzingatizi wa kanuni mbalimbali. Dhanna hizi husaidia kujibu kwa uhakika maana ya muundo virai, kwa kuzingatia kanuni.
Dhanna ya muundo virai ni kielelezo chenye vifundo vinavyounganishwa na mistari inayounda kielelezo cha matawi.
Kielelezo cha vifundo katika mchoro kinaonesha kuwa vifundo viko katika kila kategoria ya kikundi.
[S,KN,KT,KV,KH] na kategoria ya neno [N,T,V,H]. Vifundo chini ya S huitwa vifundo mama na KN na KT huitwa vifundo binti kwa S na pia KN na KT ni vifundo dada.
Kwa utaratibu huohuo T na KN ni vifundo binti wa KT lakini T na KN ni vifundo dada. H na N ni vifundo binti wa KH na pia H na N ni vifundo dada.
Kutokana na mfano wa hapo juu N,V,N,H,N huitwa vifundo tamati. Vile vingine ambavyo si vifundo vya mwisho katika kielelezo cha matawi huitwa vifundo viso-tamati. Vifundo hivi hupewa msamiati unaohusika kwa mfano katika sentensi nzima [mwalimu mkuu anafundisha darasa la nne]. Kwa kawaida vifundo viso-tamati huwa ni vile ambavyo ni vifungu yaani kwa mfano katika mchoro hapo juu [KN1, KT, KN2, KH] ni vifundo viso-tamati. Kifundo kimoja kimoja yaani viso-vifungu kama [N, V, T, N, H, N] ndiyo vifundo tamati.
Pamoja na kupewa majina, vifundo pia huelezewa uhusiano baina yake. Kuna uhusiano wa namna mbili.
- Uhusiano wa umiliki
- Uhusiano wa usabiki
Ø Uhusiano wa umiliki; unatokana na kifundo kuwa juu ya kifundo au vifundo vingine. Mfano S inamiliki KN na KT.
Kumilikiwa ni dhanna inayoelezea jinsi kifundo kimoja kinavyokuwa chini ya kifundo kingine. Kifundo cha juu kinamiliki vifundo vya chini yake. Kifundo kimoja kinasemwa kuwa kiko katika umiliki sawia [umiliki sisisi] kama kinafuatwa mara moja chini yake [bila kuwepo kifundo kingine kati yake] mfano: S inamiliki sawia KN na KT.
Kwa mantiki hii umiliki ni wa mama na binti zake. Ingawa S inamiliki pia T na KN (ya pili) kwa mbali.
Ø Uhusiano wa usabiki; huu ni uhusiano wa ki-utangulia,yaani kifundo kimoja kinasabiki kifundo kingine ikiwa kinatokea kushoto kwake. Mfano: N inasabiki V na V inasabiki vifundo T,KN,N,KH,H na N pamoja na maneno [anafundisha darasa la nne]. Kifundo kinasabiki sawia kifundo kingine ikiwa kinatokea mara moja kushoto mwa kifundo kingine. Mfano: V inasabiki sawia T na neno [anafundisha].
Kwa kutumia dhanna za umiliki na umiliki sawia tunapata istilahi mbili muhimu ambazo ni viambajengo na viambajengo vifuasi [viambajengo sisisi]. Dhanna hizi zinafasiliwa ifuatavyo:
(i) Seti ya vifundo inaweza kuunda kiambajengo iwapo na iwapo tu (iit) seti hiyo inamilikiwa na fundo moja na hakuna fundo linalosalia.
(ii) Fundo moja x huwa kiambajengo cha fundo lingine y iwapo na iwapo tu fundo hilo linamilikiwa na y.
(iii) X ni kiambajengo sisisi (sawia) cha y iwapo na iwapo tu x inamilikiwa na y.
Kielelezo hicho kinaonesha kuwa kwa kanuni ya mfuatano [D,E] haziundi kiambajengo kwa kuwa fundo moja [F] linabaki, lakini mafundo [D,E,F] yanaunda kiambajengo kimoja kwa kuwa yanamilikiwa kikamilifu na fundo C na hakuna fundo
linalobaki.
Mfano:
-Majambazi wakatili waliwaua walinzi hodari bila huruma.
T,KN2 na KH vinaunda kiambajengo [waliwaua walinzi hodari bila huruma] kwa kuwa T,KN2 na KH vinamilikiwa na fundo moja KT na hakuna fundo linalosalia. KN2 na KH haviundi kiambajengo ingawa vinamilikiwa na fundo moja [KT] kwa kuwa kuna fundo moja T [waliwaua] linasalia.
S inamiliki viambajengo vyote vilivyo chini yake [KN,KT,N,V,T,KN2,KH,N2,V2,H na N3] KN na KT ndiyo viambajengo sisisi (sawia) vya S kwa kuwa vinamilikiwa moja kwa moja na S. T,KN2 na KH ni viambajengo vya KT.
UFAFANUZI WA DHANNA YA VIFUNDO
Ø Iwapo kifundo kimoja x kinamilikiwa moja kwa moja na kifundo y basi kifundo y ni mama wa kifundo x na kifundo x ni binti wa kifundo y.
v KN1 ni kifundo mama wa vifundo N na V1 kwa kuwa vinamilikiwa na kifundo kimoja KN1
v Vifundo N1 na V1 ni vifundo dada.
v T, KN2 na KH ni dada kwa kuwa vinamilikiwa moja kwa moja na KT.
UMILIKI REJESHI
Dhanna ya umiliki imeendelea kutumiwa katika kufasili mahusiano ya miundo tata kati ya viambajengo kwa kuvihusianisha na sintaksia na semantiki.
X inamilikiwa na kiambajengo y, iwapo na iwapo tu kifundo cha mstari wa kwanza wa mchoro wa matawi unaomiliki x unamiliki pia y na x haimiliki y wala y haimiliki x.
Mfano:
Umiliki rejeshi ni umiliki wa wima na ulalo. Yaani kifundo cha juu kinamiliki vya chini yake na kifundo kilicho mstari mmoja toka kifundo cha juu kinamiliki vifundo vyote vya kulia kwake.
AINA ZA UREJESHI
Kuna aina mbili za urejeshi ambazo ni urejeshi huru na urejeshi uso huru. Urejeshi huru ni ule ambao unaweza kubainisha kikamilifu kirejelewa na urejeshi uso huru ni ule ambao hauwezi kubainisha kirejelewa kikamilifu.
Mfano:
Ø Wanafunzi wanafikiri walimu wote wanawachukia
Ø Fatuma na Ali wanajitangaza
Ø Fatuma na Ali wanatangazana
Dhanna ya urejeshi inayozungumziwa hapa ni tofauti na ile iliyozoeleka, hapa mofimu –wa-,-ji- na –an- ndizo zinazoonesha urejeshi.
1 Mofimu –wa- inaweza kurejelea kwa wanafunzi au kwa watu wengine,yaani;
v Wanafunzi wanajihisi kuwachukia walimu
v Wanafunzi wanahisi watu wengine wanawachukia walimu
Aina hii ya urejeshi ndiyo inayoitwa urejeshi huru kutokana na uhuru wa kurejelea kitajwa zaidi ya kimoja.
2 Mofimu –ji- na –an- ni urejeshi uso huru yani unarejelea Fatuma naAli na hauwezi kurejelea kitajwa kingine chochote.
Urejeshi uso-huru huwa na kisabiki ambacho kisipokuwepo inakuwa vigumu kufasilika.
Mfano:
* John wanachukia kila mmoja
Ø John na Ali wanachukia kila mmoja
Kila mmoja inaashiria zaidi ya mtu mmoja na kila mmoja haiwezi kuwa kirejeshi cha John (ambaye ni mtu mmoja tu). Kwa hiyo kanuni ifuatayo itatumika.
Umiliki fuatishi lazima uwe na kiambajengo milikishi kisabiki kinachostahili.
|
Katika dhanna ya umiliki rejeshi,kifundo kimoja kinamiliki vifundo vingine kushoto na kulia kwake ilimradi viwe katika darajia ileile. Vilevile kifundo kimoja kinamiliki vifundo vyote vinavyomilikiwa na kifundo cha kulia kwake ambacho kiko katika kiwango kilekile.
Asante
Kwakusoma MASSHELE BLOG