Sunday

MAGUFULI HOSTELI SII SHWARI USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA,NANI KUWAJIBISHWA?

0 comments
MOJA YAMAJENGO YA MAGUFULI HOSTELI YAKIONESHA UWEPO WA NYUFA 


Ikiwa ni takriban ya Wiki nne tu toka hosteli hizi kuanza kukaliwa na Wanafunzi hatimaye Nyufa kubwa na za kushangaza zimenza kujitokeza kwenye mojawapo ya
Majengo haya alimaarufu kama JOHN POMBE MAGUFULI HOSTEL Zinazo milikiwa nachuo kikuu Cha Dar es salaam .

Hosteli hizi zilizinduliwa na Mh. Rais mwanzoni mwa mwaka huu na zimeanza kukaliwa Mwezi wa 11 mwaka huu.

Ajabu ni kuwa nyufa zimezidi kuota kwenye mojawapo ya majengo haya. Hosteli hizi zimebeba takribani ya Wanafunzi 3840.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alidai kuwa majengo haya yalijengwa kwa bilioni 10 tu za kitanzania ingawa takwimu za Mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali yaani CAG waliweza kubaini kuwa majengo haya yalijengwa kwa Sh. Bilioni 54 ... Majengo haya kujengwa kwake yametumia miezi Sita tu kukamilika kwake.. Chanzo mwanahabari wetu.